VIDEO-Mashabiki Simba macho kwa Bocco, Okwi

Muktasari:

  • Simba na Azam FC zinashuka Uwanja wa Taifa leo Jumatano kwenye mchezo wa Ligi Kuu.

 Emmanel Okwi na Bocco wametengeneza pacha hatari ya ufungaji ndani ya Simba na wote kwa pamoja wamefunga jumla ya mabao 21, mawili zaidi ya yaliyofungwa na Azam (19).

Mabao yote 12 ambayo Okwi amefunga kwenye ligi amefunga katika viwanja vya Dar es Salaam.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda hakuwepo katika mechi mbili zilizopita na leo kuna hatihati ya kukosa baada ya kumia mwishoni mwa wiki katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.