Manchester City yaituliza Bristol mabao 2-1

Wednesday January 10 2018

 

England. Sergio Aguero ameipatia bao la ushindi Machester City dakika za majeruhi na kuifanya kuibuka na kifua mbele kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kombe la FA jana Jumanne usiku.

Mabao hayo mawili ya Kevin De Bruyne na Aguero yameiwezesha Manchester City kuendeleza heshima yake ya kutopoteza mechi zake.

Mashabiki wa Manchester City walilipuka kwa shangwe baada ya timu yao kupata bao la dakika za majeruhi katika dakika ya 70 kipindi cha pili.

Kutokana na umahili walioonyesha kikosi cha Bristol City, mchezo huo ulionekana ungemalizika kwa sare ya bao 1-1 hata hivyo Aguero akabadilisha upepo uwanjani hapo.

Bao la Aguero liliwamaliza nguvu Bristol City jambo lililowapunguza kasi wakati mchezo ukielekea ukingoni.