Mama Maria Nyerere aunga mkono mchezo wa bao

RAIS wa Shirikisho la Bao Tanzania (SHIMBATA),Manday Likwepa amesema wametengeza mabao mawili moja litabaki nchini na lingine litapelekwa China.
Likwepa anasema bao litakalobakia Tanzania,lina picha mbili za marais ambao ni John Pombe Magufuli na mwasisi wa nchi, Julius Nyerere.
"Nyerere ndiye mwanzilishi wa mchezo wa bao na ndio maana tumeweka picha yake katika bao hilo,lakini pia Magufuli ni mtu ambaye anapita nyendo za Nyerere na tutaenda kumkabidhi Ikulu,tukiongozwa na mama Maria nyerere."
"Bao hilo tunatarajia kulikabidhi mwishoni mwa mwezi ujao baada ya makubaliano maalumu na mama Maria Nyerere ambae amefurahia jambo hilo na amesema yeye ndiye atakayeongoza msafara huo," anasema.