Makapu: Hii sasa safi

Tuesday February 13 2018

 

By DORIS MALIYAGA

KIRAKA wa Yanga,  Said Juma 'Makapu' katika mechi za karibuni amekuwa akipewa nafasi ya kucheza zaidi beki wa kati tofauti na ilivyokuwa awali kwenye kiungo amesema, hii sasa ndiyo anayoipenda zaidi kutokana na namna anavyomudu lakini amemuachia kocha wake aamue wapi anapoona anafaa.
Makapu ambaye anajulikana ni kiungo mkabaji, lakini tangu ujio wa kocha Mzambia George Lwandamina kila kunapotokea mapungufu kwenye beki ya kati amekuwa akimchezesha  hapo.
Amesema, anapocheza hapo kwa sasa anajisikia huru na kadri mechi zinavyozidi kuongezeka ndivyo anavyokuwa imara katika nafasi hiyo.
"Awali nilikuwa napenda sana kucheza kiungo lakini sasa ninapocheza beki ya kati naona safi na kadri ninapocheza mara kwa mara napata uzoefu na kujiamini. Lakini katika yote mimi nacheza tu, walimu wangu ndiyo wanajua ni wapi panaponifaa ndiyo nimewaachia wao kila kitu,"anasema Makapu.