Liverpool yapania kutibua rekodi ya Man City

Sunday January 14 2018

 

Liverpool inashuka dimbani leo Jumapili kujaribu bahati yake mbele ya Manchester City ambayo imekuwa katika kiwango kizuri msimu huu.

Liverpool itakuwa nyumbani kulinda heshima yake huku mashabiki wa timu hiyo wakiingiwa na hofu kutokana na kasi ya City katika safu yao ya ushambuliaji.

Manchester City inaongoza msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa imejikusanyia pointi 62 na mchezo wa leo ni muhimu kwa kikosi hicho cha Etihad ili kuendelea kujiimarisha kileleni.

Kwa takribani miezi miwili sasa Manchester City haijapoteza mchezo wowote kila iliposhuka uwanjani, swali linabaki kwa Liverpool iwapo wataweza kuvunja mwiko huo.

Mchezo wa mwisho timu hizo zilipokutana msimu huu, City iliivuruga Liverpool mabao 5-0 jambo ambalo linaonyesha mchezo wa leo utakuwa mgumu  kwa Liverpool kulingana na rekodi ya City msimu huu.