Lipuli yaikomalia Azam FC

Dar es Salaam. Azam FC imepoteza nafasi ya kuisogelea Yanga baada ya kulazimishwa sare tasa na Lipuli kwenye Uwanja wa Samora mchezo uliopigwa leo Ijumaa.

Azam FC ambayo ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 baada ya kupata suluhu ya kutofungana na Lipuli FC.

Azam inatofauti ya pointi saba na Simba ambayo ipo kileleni, huku wakitofautiana pointi mbili na Yanga iliyopo nafasi ya pili.

Lipuli imesogea nafasi ya 8 imeshajikusanyia pointi 20 katika jumla ya michezo 18 iliyocheza.

Timu ambazo zinaipumulia kwa karibu Lipuli ni pamoja na Mbeya City, Stand United, Mbao FC.

Mechi zingine zitakzopigwa kesho Jumamosi Njombe itaikaribisha Majimajikwenye Uwanja wake wa Sabasaba huku Kagera Sugar itaikaribisha Singida United.

Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja kwenye Uwanja wa Sokoine ambako Mbeya City itacheza na Stand United