Leodger Tenga ateuliwa mwenyekiti mpya BMT

Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga ameteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) huku Timoth Mganga akiteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Harrison Mwakyembe kwa mujibu wa sheria ya BMT ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake amemtea Tenga kuchukua nafasi ya Dioniz Malinzi aliyemaliza muda wake.
Pia Mwakyembe amewateua wajumbe sita wa BMT ambao ni Profesa Mkumbwa Mtambo,Beatrice Singano,Kanali mstaafu Juma Ikangaa,John Ndumbaro,Rehema Madenge na Salmin Kaniki.
Waziri huyo pia wamewateua wajumbe wengine watatu wa Baraza ambao ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo,Yusuph Singo,Kamishina wa Elimu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,Edicome Shirima na Katibu mkuu wa BMT Mohammed Kiganja.