Botswana kuivaa Taifa Stars Uwanja wa Taifa leo

Muktasari:

Kikosi cha Taifa Stars, kitaongozwa na nahodha Mbwana Samatta ambaye anachezea klabu ya Genk inayoshiriki mashindano ya Ligi ya Europa hatua ya robo fainali.

Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo watakuwa wenyeji wa Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Kikosi cha Taifa Stars, kitaongozwa na nahodha Mbwana Samatta ambaye anachezea klabu ya Genk inayoshiriki mashindano ya Ligi ya Europa hatua ya robo fainali.

Stars wanatarajia kuwa na mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Burudi wiki ijayo, pia itashiriki mashindano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.

Kocha wa Pundamilia hao, Peter Butler amemjumuisha mkongwe Ofentse Nato kwenye kikosi kitakachoongozwa na nahodha wao Atletico de Kolakata.