Kocha mpya Simba atambulishwa rasmi

Dar es Salaam. Uongozi wa Simba umemtambulisha rasmi kocha mkuu mpya wa Simba kwenye mkutano uliofanyika Serena Hoteli leo jijini Dar es Salaam.

 Kocha huyo mpya, Pierre Lechantre alisaini mkataba mbele ya uongozi wa Simba kisha kukabidhiana na Rais wa Simba, Salim Abdallah.

Pia Uongozi wa Simba umetangaza kamati mbalimbali ambapo miongoni mwa kamati hizo ni

Kamati ya maadili  ambayo itaongozwa na  mwenyekiti wake Selemani Kova  pamoja na wajumbe wengine ambao ni , Robert Selasela, Asha Muhaji, Selemani Ally  na Steven Ally.

Kocha huyo mpya ametambulishwa ikiwa ni siku moja tangu akishuhudie Wekundu wa Msimbazi wakishusha kipigo kikali kwa Singida United iliyolala kwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa.