Kocha Rollers apania makubwa Afrika

Gaborone, Botswana. Kocha wa Township Rollers, Nikola Kavazovic amesema kiwango kilichoonyeshwa na timu yake dhidi ya miamba ya Sudan, Al Merrikh imeonyesha ni wazi klabu hiyo imedhamilia kuwa moja ya timu tishio Afrika.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Botswana (BPL) wamefanikiwa kuwatoa Al Merrikh kwa jumla ya mabao 4-2 katika mchezo Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na kufungwa 2-1 ugenini wamefaidika na ushindi wao wa nyumbani Gaborone wa magoli 3-0.

"Township Rollers siyo timu ya kawaida ya soka,” Kavazovic aliimbia tovuti ya klabu hiyo.

“Ni mpango wangu, mimi mwenyewe, rais wa klabu na wachezaji kwa malengo ya muda ya kuhakikisha tunakuwa moja ya timu kubwa barani Afrika. 

Al Merrikh ni moja ya klabu kubwa Afrika wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Sudan mara 16. Wamecheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa 2015.

Katika upande mwingine, Rollers inashikiria rekodi ya kutwaa ubingwa mara 14, na sasa wanataka kufuzu kwa hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.

“Imekuwa ni habari nje kwa soka la Botswana, baadhi ya watu wanafikiria kuhusu kupata pointi tatu, hata hivyo hatuna sababu ya kuwa na hofu,” alisema Mserbia huyo na kuendelea.

“Labda hatutaweza kutwaa ubingwa wa ligi, au Mascom Top 8 ua kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa; lakini tupo katika njia ya kuwa moja ya klabu kubwa Ulaya, kama siyo Afrika basi tuwe hata kusini mwa Afrika..

“Tumeonyesha hivyo kwa kuwafunga moja ya timu tano bora Afrika, Tuliwazidi kila idara na kuwaonyesha kiwango chetu kilivyo, na nidhamu yetu ya mchezo na kujilinda, kumiliki mpira na kushambulia.”

Township Rollers watacheza na Yanga katika mchezo ujao utakaofanyika kati ya Machi 6 au 7 na mshindi wa mechi hizo mbili anafuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo makubwa ya klabu barani Afrika.