Kipigo cha Chelsea kilimtoa machozi Messi

Monday February 12 2018

 

London, England. Mshambuliaji Alexis Sanchez amesema nyota wa Barcelona, Lionel Messi alimwaga chozi wakati walipotolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa na Chelsea mwaka 2012.

Katika mchezo huo Messi alikosa penalty na kufanya miamba hiyo ya Catalans ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 kabla ya Chelsea kusawazisha 2-2 wakiwa wachezaji 10 baada ya John Terry kutolewa kwa kadi nyekundu na Barca kuondolea kwa jumla ya mabao 3-2.

Sanchez ambaye katika mchezo huo alianza akiwa kikosi cha Barca, alionyesha ni jinsi gani wachezaji wenzake wa zamani wanavyoumia timu inapofungwa hasa kwa wachezaji wa kubwa.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United ambaye kwa sasa analipwa mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki ndani ya Old Trafford, pia alisema ni makosa mchezaji kushtumiwa kwa kuangalia kiasi chake cha fedha anacholipwa.

"Nafikiri soka inawasaidia wengi," Sanchez aliimbia Sky Sports. "Inakupa maisha mazuri, lakini watu hawaoni mambo yote unayopitia nyuma ya pazia.

"Hiyo haimanishi kuwa ujaiona familia yake, au umeshindwa kwenda kusherekea siku ya kuzaliwa mama yako, wachezaji wengi wanatazama kama wameshindwa kusherekea siku za kuzaliwa watoto wao.

"Unaweza kulia unapopoteza mchezo. Hayo yote ni sehemu ya mchezo. Nakumbuka tukiwa Barcelona baada ya mechi dhidi ya Chelsea, nilimuona Messi akilia. Hiyo ni kwa sababu alikuwa anataka mambo makubwa. Watu hawaoni hayo.