Kilimanjaro Marathon kuvunja rekodi ya wanariadha

Monday February 12 2018

 

By Yohana Challe

Arusha: Mashindano ya Kilimanjaro Marathon yanayotarajia kufanyika Machi 4 mwaka huu Mkoani Kilimanjaro yatashirikisha zaidi ya wanariadha 10,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.

 Mratibu wa Mashindano hayo John Bayo alisema mwaka jana walishirikisha wanariadha 9,500 huku mwaka huu wakitarajia kuvuka idadi hiyo ili kuendelea kuwa moja ya mbio bora siyo Tanzania pekee bali Afrika.

 “Kinachofanyika kwa sasa ni kumalizia mambo machache yaliyosalia kwenye uandaaji na zoezi la kujiandikisha litaanza Jijini Dar es Salaam Februari 27 pale Mlimani City kabla ya kuhamia Arusha na mambo yote yatakuwa yakifanyika Moshi siku za mwisho” alisema Bayo.

 Aliongeza kuwa mbio za mwaka huu hazijabadilika utaratibu kama miaka ya nyuma kila mshiriki atalazimika kujiandikisha mapema ili kupata namba ya ushiriki ndio kigezo kitakachoangaliwa.

 “Kuwa kuhakikisha tunanyajua uchumi wa wanariadha wetu na kuwatangaza tayari tumewatafutia mashindano Afrika Kusini yale ya Cape Town Marathon yatakayofanyika Juni baada ya mambo kukaa vyema kila kitu tutaweka wazi”

 Bayo alisema kama Mtanzania hata maliza wa kwanza kwenye mashindano hayo bado wanayo nafasi kwa wale watakaofanya vizuri wawili wanawake na wawili wanaume ndio watakaopata nafasi hiyo.