Kilichomuua mama mzazi wa msanii Johari hiki hapa

Muktasari:

Chiki Mchome ambaye ni msemaji wa familia, alisema mazishi yatakuwa kesho saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu na kabla ya maziko hayo mwili utaswaliwa katika, Msikiti wa Masjid Maamur uliopo Upanga.

Dar es Salaam. Muigizaji filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amefiwa na mama yake mzazi leo Jumatano katika Hospitali ya Hindu Mandal, alipokuwa anatibiwa kutokana na kusumbuliwa na presha kwa muda mrefu.

 Johari alisema ameupokea msiba huo kwa mshtuko na umemuumiza. “Kiukweli nimeumia sana na pia namshukuru mwenyezi Mungu kwa kuweza kunipa nguvu ya kushiriki katika msiba huu wa mama yangu mazazi.”

“Mama alikuwa anasumbuliwa na presha ya muda mrefu, ilikuwa inakuja na kutulia, lakini tangu jana hakuwa vizuri, hadi leo mauti yanamkuta na kesho tunatarajia kumzika kwani mama yangu alikuwa ni Muislamu,” alisema Johari.

Kwa upande wa Chiki Mchome ambaye ni msemaji wa familia, alisema mazishi yatakuwa kesho saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu na kabla ya maziko hayo mwili utaswaliwa katika, Msikiti wa Masjid Maamur uliopo Upanga.

“Tulikuwa na kikao na ndugu wa familia ya msanii mwenzetu Johari, ambaye amefiwa na mama yake mzazi na ratiba ya maziko yatakuwa ni kesho katika makaburi ya Kisutu, mwili utaswaliwa katika Msikiti wa Masjid Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam,” alisema Chiki.