Kapombe kuliamsha kwa Kagera Sugar

Muktasari:

Beki huyo amekuwa nje ya uwanja tangu alipojiunga na Simba akisumbuliwa na matatizo mbalimbali

Kagera. HATIMAYE beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe ameingia kwenye kikosi cha wachezaji 18 watakaocheza dhidi ya Kagera Sugar leo Jumatatu jioni

Kapombe hajawahi kuingia kwenye orodha ya wacheza 18 wa mchezo tangu aliposajiliwa na Simba mwezi Julai mwaka Jana.

Beki huyo wa zamani wa Azam amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 5 akiuguza majeraha mbalimbali, jambo ambalo limemfanya ashindwe kuitumikia timu yake hiyo mpya.

Wakati huo huo, kiungo Said Ndemla ameingia kwenye kikosi cha kwanza leo baada ya kuonyesha kiwango bora dhidi ya Singida United.

Kikosi cha Simba leo kitakuwa

Aishi Manula, Nicolas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid,  Erasto Nyoni , Jonas Mkude,  James Kotei, Said Ndemla, John Bocco, Shiza Kichuya, Emmanuel okwi

Wachezaji wa Akiba

Kipa Emanuel Mseja,  Mohammed Hussein, Muzamir Yassin, Yusufu Mlipili, Shomari Kapombe, Laudit Mavugo na Mwinyi Kazimoto