Kagera Sugar, Simba waijaza mapema Kaitaba

Muktasari:

Simba inashuka kwenye uwanja huo ukiwa na kumbukumbu ya kufungwa hapo msimu uliopita

Kagera. Bila kujalisha kwamba ni siku ya Jumatatu, maelfu ya mashabiki Wa soka mjini hapa tayari wamejaza majukwaa ya uwanja Wa Kaitaba masaa mawili kabla ya Kagera Sugar na Simba mechi kuanza.

Timu hizo mbili zinakutana miezi saba baada ya Kagera kushinda 2-1  katika mchezo Wa mwisho ambao baadaye ulileta kizungumkuti nje ya uwanja baada ya madai kwamba beki wa Kagera, Mohammed Fakhi alikuwa na adhabu ya kadi tatu za njano.

Mashabiki wa Simba ndiyo wamefurika kwa wingi uwanjani hapa ikiwa ni juhudi za kuongeza hamasa kwa timu yao ambayo inausaka ubingwa kwa mwaka wa sits sasa bila mafanikio.