Kabwili amshangaza kocha

Tuesday February 13 2018

 

By DORIS MALIYAGA

KOCHA mkuu wa St Luois ya Shelisheli, Michel Reneeud  alipomwona mlinda mlango wa Yanga,  Ramadhan Kabwili akawashangaa watoto hao wa Jangani kumwamini golini, lakini akapongeza kitendo hicho na kusema atakuja kuwa mzuri zaidi hapo baadaye.
Kabwili alidaka kwenye mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika walipocheza na St Luois hatua ya awali wakatoka na ushindi wa bao 1-0.
Reneeud anamjua Kabwili alimwona kwenye timu ya taifa ya vijana (U-17) walipocheza na Shelisheli ndiyo maana alishangaa kumwona kwenye kikosi hicho cha Jangwani.
"Huyu ni Kabwili namjua huyu kipa, nimeshangaa kumwona hapa ni mdogo Yanga wamemwamini yeye. Nilimwona alipokuja Shelisheli na timu ya vijana wamempa timu kubwa,"anahoji na kuongeza.
"Nimeshangaa sana, lakini kitu ninachoamini, atakuja kuwa kipa mzuri sana hapo baadaye kutokana na hiki wanachokifanya,  kikubwa kama na yeye atathamini, atakuja kuwa mchezaji mzuri zaidi baadaye."