Jezi ya Seseme yazua maswali Mwadui

Muktasari:

Kiungo Seseme amekuwa nje ya uwanja akisumbuliwa na tatizo la goti

Arusha: Kiungo wa Mwadui, Awesu Awesu ameeleza sababu iliyowafanya waingia uwanjani na jezi ya mchezaji mwenzao Abdalah Seseme katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare 2-2 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

 Awesu alisema waliamua kufanya kitendo kile kwa ishara ya kumtakia kila la kheri Seseme apata kupona haraka na aweze kurejea uwanjani.

 “Afya ya Seseme siyo nzuri na imekuwa ikituumiza kila tunapomkumbuka kwa kuwa ni mchezaji ambaye amekuwa ni kipenzi cha kila mtu hapa kambini hivyo kukosekana kwake ni pengo kubwa siyo uwanjani tu” alisema Awesu.

 Aliongeza sababu ya yeye kupewa kushika jezi hiyo ni kutokana na kuwa mtu wake wa karibu zaidi kama vile