T: Jezi ya Okwi, Bocco, Tshishimbi ni neema tupu

Muktasari:

Changamoto kubwa ni Simba na Yanga  ni kushindwa kufaidika kwa mauzo ya jezi

Shinyanga. Jezi ya Emmanuel Okwi, John Bocco, Asante Kwasi na Papy Tshishimbi zimeendelea kuwafaidisha wafanyabiashara wa jezi katika mikoa mbalimbali nchini.

Tangu asubuhi maeneo ya karibu ya Uwanja wa Kambarage mashabiki wamekuwa wakigombea kununa jezi zenye majina ya wachezaji hao.

Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba leo wapo Shinyanya kuwavaa wenyeji wao Mwadui katika mchezo utakaochezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kambarage mjini hapa.

MCL digital imepiga kambi mjini shinyanga, imeshuhudia asubuhi wafanyabiashara wakipishana na jezi nyekundu katika mji huo, huku wengi wao wakisema biashara kwa sasa ni safi kutokana na ushindi wanaoupata Simba kila mechi.

Mmoja wa wafanyabiashara, Othmana Madoshi amesema jezi nyekundu kwa sasa ni diri na jina la Okwi, Bocco na Kwasi ameziuza sana.

"Ni sawa hata za Yanga zinauzwa kama Tshishimbi, lakini za Simba zinauzwa kwa sana, jezi haswa za Okwi, Bocco na Kwasi ambaye watu wanampenda kwakuwa ni mpya,"amesema Madoshi.

Wakati huohuo, mashabiki na wadau wa soka tayari wamejazana mlangoni kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo.