JKT Tanzania yaikamia Ndanda

Muktasari:

JKT Tanzania imebadilisha jina lake zamani ilijulikana na JKT Ruvu

 

 

Dar es Salaam. Timu ya JKT Tanzania imeendelea na maandalizi yake ya mchezo wa Kombe FA dhidi ya Ndanda kwenye Uwanja wa Mbweni.

Timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu huu ipo chini ya kocha wake Bakari Shime 'Mchawi Mweusi' ikiwa na lengo la kuendeleza rekodi yake nzuri ya ushindi msimu huu.

JKT Tanzania imefuzu kwa hatua hiyo ya 16 bora baada ya kuichapa Polisi Dar bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya 32 iliyofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.

Katika mazoezi hayo, Shime alikuwa na wachezaji wake nyota Hassan Matelema, Samweli Kamutu, Rahimu Juma na Salim Gila.

Kocha wa JKT Tanzania, Shime alisema mazoezi katika jua kali imekuwa ni silaha yake katika maandalizi yao.