IRFA yachukua Lipuli

Iringa. Chama cha Soka Mkoa wa Iringa (IRFA) kimeingilia kati mgogoro ulioikumba Lipuli FC kwa kuamua kuichukua timu hiyo kwa muda.

Akitangaza uamuzi huo aliodai una baraka zote za serikali ya mkoa wa Iringa,  Mwenyekiti wa IRFA, Cyprian Kuyava alisema kuanza sasa timu itakuwa chini cha chama hiyo na wataunda kamati ya muda ya kuisimamia hadi hapo mgogoro utakapomalizika.

Alisema lengo la mpango huo ni kuinusuru na janga la kushindwa kufanya maandalizi mapema ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu ujao.

 “Sisi ni walezi wa timu zote, tumesikitishwa na mgogoro huu uliotokea mara tu baaa ya Lipuli FC, kupanda Ligi Kuu, tumewaeleza Rais wa TFF, Jamali Malinzi na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi wote wameelezea kusitishwa kwao na jambo hili,”alisema Kuyava.