Fellaini amgomea Mourinho

Tuesday January 9 2018

 

Kiungo Mbelgiji amekataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Manchester United na sasa yuko huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote ili akajiunge nayo mwisho wa msimu huu.

Kocha wa Manchester United, Mourinho alikuwa na lengo la kutumia kipindi cha wiki moja cha kambi ya Dubai kumshawishi Fellaini kuendelea kubaki United. Lakini uamuzi wa Fellaini ni kuhamia katika klabu nyingine.

Man United inatarajiwa kurejea England kuikabili Stoke City, baada ya kupata mapumziko  ya wiki moja nchini humo.

Mourinho amepanga kumshawishi Fellaini kwa kumpa nyongeza ya mshahara katika maboresho ya mkataba wake.

Man United imeweka mezani mkataba wa miaka miwili na mshahara wa Pauni120 milioni kwa wiki lakini dau hilo linaweza kuongezeka.

Fellaini alirejea uwanjani tangu alipocheza mara ya mwisho Novemba 25 kabla ya kuingia dakika za majeruhi akitokea benchi katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Derby County katika Kombe la FA. Hakucheza mechi 11 kutokana na na jeraha la kifundo cha mguu.