Falcao aamsha hasira za Balotelli

Muktasari:

Monaco na Nice zilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa Ligue 1 uliopigwa jana Jumanne usiku.

Mashambuliaji wa Nice, Mario Balotelli aliifungia klabu yake mabao mawili dhidi ya Monaco kwenye mchezo uliopigwa jana Jumanne usiku Uwanja wa Stade Louis II, mchezo ulioisha kwa sare ya mabao 2-2.

Bao la usiku la Radamel Falcoa lililofungwa dakika ya nyongeza baada ya 90 za kumalizika lilizima ndoto za Mario Balotelli kuipa pointi tatu klabu yake ya  Nice baada ya kufungwa bao la kusawazisha dakika za majeruhi.

Mabao yote mawili ya Ballotelli yalifungwa kwenye kipindi cha pili huku akijiweka kwenye nafasi nzuri ya kuziona nyavu ikiwa ni ushindi wake mkubwa kwa mcherzo wa jana.

Mpaka sasa Baloteli amefunga mabao 10 kwenye mechi 10 alizoichezea Nice kwenye mashindano yote.