Eneka ya Diamond yaishika Djibout

Muktasari:

Diamond amekuwa na mafanikio makubwa katika soko la muziki barani Afrika kwa sasa

Djibouti City, Djibout. Mwanamuziki Diamond ameiteka Afrika kwa sasa si nyumbani tu, kwani huku Djibouti ndiyo habari ya mjini anatesa na wimbo wake wa Eneka.

Tena huku hajulikani kwa sababu ya misukosuko yake mapenzi ya wakina Wema Sepetu, Amisa Mabeto na Zali, kwa nyimbo tu.

Mwanaspoti limetia timu nchini Djibouti na lilipowasili kwenye hoteli ya Sheraton walipoweka kambi wachezaji wa Simba na wafanyakazi wa hapo walipojua Simba wametoka Tanzania wakakazia anapotoka yule mwanamuziki Diamond.

Mmoja wa wahudumu wa hotelini hapo aliyejitambulisha kwa jina la Awo alisema, anampenda msanii huyo na anavutiwa na wimbo wake wa Eneka.

Hata kwenye ndege waliyosafiria Simba ya KQ walipojua kikosi hicho kinatoka Tanzania waliuliza, mbona hamjambeba na yule msanii, Diamond.