De Gea sasa kuzeekea Man United

London, England. Kipa David De Gea yuko mbioni kusaini mkataba mpya Old Trafford wenye thamani wa pauni 220,000 kwa wiki ili kuendelea kubaki  Manchester United.

Mhispania huyo kwa mara nyingine amehusishwa kutakiwa na Real Madrid, lakini tayari kumekuwa na mazungumzo yanaendelea ya kuongeza mkataba mpya Old Trafford utakaompa mshahara wa pauni 220,000 kwa wiki.

Gazeti la The Times limeripoti kuwa Man United wanataka kubaki na kipa huyo hadi mwaka 2021.

De Gea alionyesha kiwango cha juu wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sevilla uliomalizika kwa suluhu katika hatua ya 16 bora.

Hakuna ubishi kuwa jina la kipa huyo kwa sasa limejihakikishia namba katika kikosi cha Jose Mourinho na kiasi cha kuamua kuongezea mkataba mpya.