Chirwa ana siri nzito Yanga

STRAIKA wa Yanga, Obrey Chirwa amefunguka na kwamba anachokifanya huwa ana sababu na si mjinga kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Chirwa ambaye anatumikia kifungo cha mechi tatu alichopewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu, alisema katika maisha amejifunza jambo moja muhimu la kusimamia anachokiamini.

“Maisha yangu yako hivyo, wengi wananiona wa tofauti au mkorofi ila naishi hivyo. Sipendi masihara, sipendi blah blah, napenda kila kitu kiende sawa,” alisema Chirwa aliyeifungia Yanga mabao sita msimu huu.

“Kutokana na hilo, imekuwa vigumu kumwamini mtu yeyote kwa sababu unaweza kufanya jambo fulani usieleweke, yule unayemwamini ndiyo atakuja kukufanya vibaya na kuwa adui yako.”