Buswita arejesha kicheko Jangwani

Muktasari:

Katika kipindi cha kwanza timu zote zilionekana kucheza kwa kujiwinda, lakini Yanga walipata bao dakika ya 45, Pius Buswita aliifungia bao Yanga baada ya kuonganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Ibrahim Ajib.

KIKOSI cha Yanga kimerejesha furaha kwa mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Ruvu Shooting.
Katika kipindi cha kwanza timu zote zilionekana kucheza kwa kujiwinda, lakini yanga waliweza kupata bao dakika ya 45, Pius Buswita aliifungia bao Yanga baada ya kuonganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Ibrahim Ajib.
Katika kipindi cha pili timu zote zilifunguka na kucheza mpira, huku Ruvu Shooting wakionekana kufika mara kwa mara golini mwa Yanga kupitia kwa straika wao Issa Kanduru.
Mabadiliko ya yanga katika dakika 26 Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Yohana Mkomola na kuingia Emmanuel Martin, mabadiliko ambayo yalionyesha uhai kwa Yanga.
Shooting nao walifanya mabadiliko dakika 49 baada ya kumtoa Ayoub Kitala na kuingia Full Zully kwani ilifanya mchezo kuwa wa kushambuliana muda wote.