Jamani Aunty halipendi jina hili la Mkata Viuno

Friday February 17 2017

 

By HERIETH MAKWETTA

MWIGIZAJI nyota wa kike nchini, Aunty Ezekiel amesema katika kipindi chote alichokuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Moses Iyobo, kitu kikilichokuwa kikimuudhi na kumuuma ni kuambiwa anatoka na Mkata Viuno.

Aunty alisema kwa mara ya kwanza analisikia hilo neno aliumia sana lakini hakuwa na jinsi.

“Kusema kweli kuna mambo mengi yanatokea kwenye uhusiano wetu, lakini mimi hakuna kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza kama watu kuniambia natoka kimapenzi na Mkata Viuno, nilikuwa naumia sana kusema kweli.

“Ila baadaye nikawa nashangaa haohao waliokuwa wananikejeli kuwa natoka na Mkata Viuno wakaanza kumtumia meseji Mose wakimtaka kimapenzi, lakini nashukuru sikukata tamaa mpaka sasa nipo na Mose na tunapendana sana,” alisema Aunty.

Aunty alisema amevumilia vitu vingi mpaka sasa na anayafurahia maisha yake akiwa Iyobo ambaye ni dansa wa, Diamond Platnumz.