JB, Wema wapelekwa rasmi nchini China

Muktasari:

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye aliwaombea wasanii hao kwa serikali ya China ambapo maombi hayo yalipokewa kwa mikono miwili.

WASANII wa Filamu za Kibongo wamepewa fursa ya kuanza kuuza filamu zao nchini China ambao sasa zitakuwa zikitafsiriwa kwa lugha ya nchi hiyo kama ambavyo Rufufu amekuwa akitafsiri za kwao hapa nchini.

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye aliwaombea wasanii hao kwa serikali ya China ambapo maombi hayo yalipokewa kwa mikono miwili.

Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini, Simon Mwakifwamba alisema wamepanga kuanza kutengeneza filamu zenye viwango vya juu ili kuweza kukimbizana na soko hilo lenye idadi ya watu zaidi ya bilioni moja.

China imezindua wiki ya filamu zake hapa nchini ambapo kazi hiyo inasimamiwa na kampuni ya ving’amuzi ya Star Times ambapo uzinduzi huo ulifanywa na Nnauye Jumatano jioni.

Hata hivyo jana Alhamisi asubuhi nafasi yake ya uwaziri katika wizara husika ilitenguliwa.