Mastaa wapya wenye mvuto Nollywood

Tuesday March 12 2013Benson Okonkwo

Benson Okonkwo 

By new

LAGOS, NIGERIA KUKUA kwa tasnia ya filamu nchini Nigeria kumechochea kwa kiasi kikubwa kuibuka kwa chipukizi wapya kila uchao wanaojaribu kufanya mapinduzi ya sanaa. Sura za akina Omotola, Genevieve, Mercy Johnson, Jim Iyke, Desmond Elliot, Emeka Ike na wengine wa daraja lao zimekuwa zikipotea taratibu. Hii imesababishwa na kuja kwa kasi kwa mastaa wapya ndani ya Nollywood. Sura hizi mpya sio tu ni vijana bali wako vizuri kila idara. Unaweza kusema wamejaaliwa uzuri, mvuto na pia vipaji vya hali ya juu. Vijana hawa wamekuwa wajishindia mataji mbalimbali katika mashindano kadhaa wanayoshiriki. Hii inaonyesha dhahiri ni kwa vipi watu hawa wana vipaji vilivyoshiba. Hawa ni wenye mvuto zaidi kwa upande wa wanaume: Michael Okon Michael Okon ni miongoni mwa makinda wapya wanaofanya vizuri ndani ya Nollywood. Kwa mara ya kwanza kabisa alikuja kwenye filamu ya ‘Fragile Pain’ ambapo aliigiza kama mtu aliyevurugwa na mwanasiasa mmoja tajiri na mwenye uchu wa madaraka. Kwa kuitendea haki filamu hiyo, aliweza kupata nafasi katika kazi nyingine zilizofuatia kama vile ‘African Queen’, ‘Men Do Cry’ na nyingine nyingi. Junior Pope Odonwodo Tangu aingie rasmi kwenye tasnia ya filamu mwaka 2008, Junior Pope Odonwodo, ameweza kufanya kazi nzuri zaidi jambo lililochangia kumfanya akae kwenye chati kwa muda mrefu sasa. Mwigizaji huyu amekuwa kipusa na hadi sasa tayari amefanya kazi kibao. Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na ‘Kingdom of Beauty’ na 'Mad Sex'. Alex Ekubo Baada ya kushiriki shindano la ‘Mr. Nigeria’, Alex Ekubo, moja kwa moja alijitosa kwenye uigizaji na uanamitindo. Hivi sasa amekuwa akionekana kuja juu zaidi kwenye uigizaji. Kutokana na uwezo aliokuwa nao, amekuwa akionekana lulu miongoni mwa waigizaji wa kiume chipukizi ndani ya Nollywood. Uti Nwachukwu Kwa wale wanaofuatilia shindano la Big Brother, jina Uti Nwachukwu litakuwa si geni masikioni mwao. Baada ya kunyakua taji hilo mwaka jana, Uti aliamua moja kwa moja kuingia kwenye fani ya uigizaji wa filamu na utangazaji. Mwaka 2010 alitokea kwenye filamu yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la ‘True Citizen’. Kutokana na kukubalika kwa kazi yake hii ya kwanza aliweza kuigiza kwenye filamu nyingine kibao. Gbenro Ajibade Unapotaja mastaa wapya wa Nollywood wenye vipaji lukuki huwezi kulikosa jina la Gbenro Ajibade Emmanuel. Yeye ni mtangazaji wa Televisheni, mwanamitindo wa kimataifa na pia mwigizaji. Anaigiza kwenye tamthilia ya ‘Tinsel’ ambayo inaonyeshwa hivi sasa katika nchi 72 za barani Afrika na Ulaya. Benjamin Joseph Umaarufu wake ulizidi kujengeka pale alipopata nafasi ya kuendesha shindano maarufu la MTN Project Fame. Joseph Benjamin amekuwa gumzo katika fani hiyo ya uigizaji hususani katika Nollywood. Mvulana huyu mtanashati na mwenye mvuto, amezidi kujizolea umaarufu kwenye tasnia ya filamu. Hivi karibuni alikuja katika filamu mpya inayofahamika kwa jina la ‘Mr. and Mrs’ ambapo aliigiza nafasi ya mume mkorofi huku nafasi ya mke wake ikiigizwa na Nse Etim-Ekpe. Kenneth Okolie Kenneth Okolie ni mshindi wa zamani wa taji la Mr Nigeria. Hivi karibuni aliripotiwa kutekwa akiwa katika kazi pamoja na mwigizaji mwenzake Sylvanus Nkiru. Ken anatajwa kuwa miongoni mwa waigizaji chipukizi wanaokonga nyoyo za wapenzi wa filamu za Kinigeria. OC Ukeje Wapenzi wa filamu za Kinigeria watakubaliana na ukweli kuwa O.C. Ukeje ni mwigizaji wa kipekee. Mambo aliyoyafanya kwenye filamu za 'Gone Too Far', 'Half Of A Yellow Sun' na 'Till Death Do Us Part', yanatosha kabisa kujua uwezo wake. Ni mwigizaji mahiri mwenye uwezo mkubwa wa kuigiza katika sehemu tofauti tofauti. Sababu hii na nyingine ndio zinazochangia kwa kiasi kikubwa kumuweka juu. Gideon Okeke Kama ilivyo kwa Gbenro Ajibade, naye Gideon Okeke ni mtangazaji, mwanamitindo na mwigizaji. Anaigiza katika tamthilia ya ‘Tinsel’ na pia amewahi kuigiza kwenye tamthilia ya ‘Relentless’ ambayo ilikuwa ikirushwa mwaka 2010. Benson Okonkwo Anatajwa kuwa miongoni mwa wavulana watanashati ndani ya Nollywood. Kama vile haitoshi unaweza kumwelezea kutokana na uwezo na kipaji alichonacho katika suala zima la sanaa. Kazi iliyompa heshima ni ‘Desperate Hawkers’ . Inasemekana ndicho chanzo cha yeye kupata kazi nyingi zaidi