Burudani

Eti Jack Wolper naye ni Bosslady!

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

 

Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Ijumaa,Februari17  2017  saa 14:46 PM

MWIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Jacqueline Wolper amesema kuwa kwa sasa ni mwanamke maalumu anayejiweza kwa kila kitu, hivyo hana sababu ya kuendesha gari.

Staa huyo anayesifika kwa kubadilisha viwalo kila uchao, alisema kwa kuwa kwa sasa ni mwanamke wa shoka anayemiliki fedha na vitega uchumi ikiwemo maduka ya nguo haoni sababu ya kuhangaika barabarani kujiendesha.

“Mimi ni bosslady bwana, naendeshwa na dereva wangu, kwanza mwanamke unaendeshaje gari kwa mfano, siwezi kushika usukani na kuendesha wakati dereva yupo,” alisema Wolper.

Hata hivyo, mwanadada huyo ambaye anasemekana ametemana na aliyekuwa mpenzi wake mwimbaji wa Kundi la Wasafi (WBC), Harmonize, alipoulizwa kuhusu jambo kutemana na mchuchu wake huyo, alisema hayupo tayari kuzungumza zaidi suala hilo kwa sasa.