Nay sasa ni mwendo mdogo mdogo

Muktasari:

Nay aliyasema hayo katika mahojiano na Mwanspoti kuhusu kolabo yake na wanamuziki kutoka Nigeria, ambao taarifa zilizozagaa ni kwamba anataka kufanya nao video yenye gharama ya Sh60 milioni.

RAPA wa muziki wa Hiphop nchini Nay wa Mitego amesema katika kazi zake za muziki anapendelea kufanya mambo chini chini.

Anasema hapendi kutangaza kazi kabla haijakamilika.

Nay aliyasema hayo katika mahojiano na Mwanspoti kuhusu kolabo yake na wanamuziki kutoka Nigeria, ambao taarifa zilizozagaa ni kwamba anataka kufanya nao video yenye gharama ya Sh60 milioni.

Alisema hawezi kuweka mambo hadharani kwani wasanii wengi wamekuwa na tabia ya kutangaza matarajio yao kabla ya kuyakamilisha suala ambalo huwaharibia pindi wanaposhindwa kukamilisha malengo yao.

Nay anayetamba na wimbo ‘Akadumba’ amesema hiyo itakuwa ni mara ya tatu kufanya kazi nje ya nchi tangu alipofanya video mbili ikiwamo ‘Nakula Ujana’ na ‘Mr Nay’.
“Tukubali, tukatae wenzetu Nigeria wapo mbali sana kimuziki na wametupita katika vitu vingi, nimeamua kuwashirikisha kwa kuwa naamini tukikutana tutafanya kitu ambacho ni kizuri zaidi,” alisema Nay wa Mitego.

Kwa mujibu wa Nay video hiyo itatengenezwa Afrika Kusini chini ya prodyuza God Father.