Lady Jaydee ataja sifa za mpenzi mpya

Muktasari:

Jaydee alitaja sifa za mpenzi huyo na kuweka wazi kwamba anataka mtu ambaye atamheshimu na kumtunzia utu wake.

ILIKUWA ni wiki la kipekee kwa mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ baada ya kukubali kujibu maswali ya mashabiki wake katika matandao wa Instagram, ambapo jana alifunguka kuhusu mpenzi anayemuhitaji kwa sasa.
Jaydee alitaja sifa za mpenzi huyo na kuweka wazi kwamba anataka mtu ambaye atamheshimu na kumtunzia utu wake.
“Anayejali na kuheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma anayeweza kuniangalia na kuniwezesha kifedha, asiyechepuka hovyo, asiwe tegemezi hata kama siyo tajiri lakini asinitegemee. Asiwe mlevi kupindukia wa kulala baa, wala kulala nje kwa machangudoa wa Kinondoni wala popote pale, nikikohoa tu awepo hapo,” alisema Jaydee.
Alipoulizwa kama ana uhusianoa kwa sasa alijibu; “Nashindwa kutofautisha kati ya boyfriend na Lover wanaojua Kizungu wanaweza kunisaidia, ila kama ni kwa maana ya rafiki wa kawaida wa kiume ninaye na si pekee nina marafiki wengi sana wa kiume kuliko wa kike, swali kuhusu ndoa nitalijibu Ijumaa (kesho) na ndiyo litakuwa swali la mwisho.”