Lulu hata hajielewi kabisa

Tuesday April 16 2013Lulu

Lulu 

By new

MSANII wa filamu, Lulu, ametamka kwamba hakuwahi kufikiria kwamba kwenye maisha yake atakumbana na majaribu makubwa kama anayopitia kwa sasa. Msanii huyo hivi karibuni aliachiwa kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili akituhumiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii maarufu, Steven Kanumba. Lulu alikuwa katika simanzi kubwa wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Kanumba iliyofanyika jijini Dar es Salaam na alishindwa hata kuzungumza kwa kirefu. Msanii huyo alionekana mwenye mawazo na anayekumbuka vitu vingi kuhusu marehemu. ìSikuwahi kufikiria hata siku moja kama naweza kupitia katika mapito kama haya,î alisema Lulu huku akilia kwa uchungu. Kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha Kanumba kitokee ilifanyika katika Kanisa la KKKT Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita kwa ibada kisha wasanii kushiriki katika chakula cha mchana kabla ya kuelekea makaburini na baadaye kuhamishia shughuli hizo viwanja vya Leaders.