Burudani

Jamani! Mariam wala hataki skendo

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

Mariam Ismail 

By new  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Jumanne,Aprili16  2013  saa 24:0 AM

MARIAM Ismail amedai kuwa hahitaji skendo ili kujiongezea umaarufu kama wanavyofanya wasanii wenzake wa Bongo. "Binafsi sihitaji skendo ili niwe maarufu bali ninachofahamu ni uwajibikaji katika kazi ninayopewa na mtayarishaji wa filamu husika, ninachohitaji ni kusoma muongozo (script) vizuri kisha kuvaa uhusika kulingana na nafasi nitakayopewa kuigiza," alisema. "Mara nyingi wasanii tunahitaji hisia, hicho ndicho ninachofanya katika filamu zote nilizoigiza na kunifanya niwe bora." Msanii huyo ameshiriki katika filamu kadhaa zikiwamo 'Best Man', 'Wrong Decision', 'Identical', 'Samatha' na 'Doa La Ndoa'. Msanii huyo ni matunda ya kazi ya Mtitu kutoka 5 Effect ambaye mara nyingi hukuza vipaji vya filamu Bongo, makali ya Mariam yanafananishwa na ya mwigizaji wa kike wa Nigeria, Omotola Jalade.