Bocco aibadili Simba Djibout

Muktasari:

Simba walizoeleka kucheza mfumo wa 3-5-2, lakini kutokana na kuumia kwa Bocco kumemlazimisha kocha Pierre Lancharte kutumia mfumo wa 5-4-1.

Dar es Salaam. Benchi la ufundi la Simba, limelazimika kubadili mfumo wake wa uchezaji, baada ya mshambuliaji wao John Bocco kushindwa kupoka kwa wakati kabla ya mechi ya leo jioni dhidi ya Gendarmarie ya Djibout.

Simba walizoeleka kucheza mfumo wa 3-5-2, lakini kutokana na kuumia kwa Bocco kumemlazimisha kocha Pierre Lancharte kutumia mfumo wa 5-4-1.

Mfumo huu umeharibika baada ya pacha wa Emmanuel Okwi, Bocco kuumia hivyo inaonekana dhahiri klabu hiyo imeamua kujilinda kuliko kutafuta bao, japokuwa katika benchi la wachezaji kuna mshambuliaji chipukizi Moses Kitandu.

Mfumo wa Simba katika safu ya ulinzi, umekuwa na mabadiliko safari hii baada ya Nicholas Gyan kurejea huku Shomari Kapombe akikosekana katika kikosi hicho, huku mabeki wengine wakiwa Juuko Murshid, Yusuph Mlipili, Asante Kwasi,Erasto Nyoni.

Katika nafasi ya kiungo ameweka viungo watano, James Kotei, Jonas mkude, Mzamiru Yassin na shiza Kichuya, huku wakimsimamisha mbele Emmanuel Okwi kama mshambuliaji pekee.

Hata hivyo, Simba wanakuwa na kawaida ya kuwatumia mabeki wao kama mawinga, hivyo utakuwa mtaji mzuri kwa Simba kumtumia Kichuya kama msaidizi wa Okwi.