Bao la Wanyama laiteka England

Muktasari:

Kiungo huyo amerejea kwa kishindo katika kikosi cha Spurs akitokea katika majeruhi

LONDON, ENGLAND. Bao lile matata kabisa la Victor Wanyama alilowafunga Liverpool limechaguliwa kuwa Bao Bora la Mwezi Februari kwenye Ligi Kuu England.

Kwenye mechi hiyo ambayo kiungo huyo wa kimataifa wa Kenya alitokea benchi kuja kuisaidia Tottenham Hotspur kupata sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool, alifunga kwa shuti kali lililowaduwaza wengi na kutinga wavuni kwa kupitia kwenye kona ya goli la Liverpool.

Straika Harry Kane alikosa penalti moja na kufunga nyingine kati ya mbili ilizopata Spurs, huku Liverpool wao mabao yao yote mawili yalifungwa na staa wa Misri, Mohamed Salah. Wanyama alifunga bao lake katika dakika ya 80 ya mchezo.