Banda ana siri nzito

Muktasari:

Banda, ambaye amekuwa beki tegemeo wa Baroka FC ya Afrika Kusini tangu alipojiunga mwaka jana akitokea Simba, alisema maisha ya nje ya nchi yana tofauti kubwa na unapokuwa nyumbani hivyo, ni lazima akili ifanye kazi kwa haraka.

BEKI wa Taifa Stars, Abdi Banda amesema ni fahari kubwa kwa mchezaji kucheza soka la kulipwa nje, lakini nidhamu na adabu vinahitajika kwa kiwango cha juu kutokana na mazingira kuwa tofauti.

Banda, ambaye amekuwa beki tegemeo wa Baroka FC ya Afrika Kusini tangu alipojiunga mwaka jana akitokea Simba, alisema maisha ya nje ya nchi yana tofauti kubwa na unapokuwa nyumbani hivyo, ni lazima akili ifanye kazi kwa haraka.

“Kwanza unapoishi mbali na nyumbani ni darasa tosha kwako, kwa sababu inahitaji uvumilivu wa hali ya juu na hiyo itakufanya uwe na akili kubwa pamoja na nidhamu ya hali ya juu.

“Hii ni kwa sababu unakutana na watu tofauti na unaishi katika mazingira ya watu wengine tofauti na yale uliyoyazoea na hiyo ndiyo changamoto kubwa ambayo wengi inawashinda na kuamua bora maisha ya kucheza mpira nyumbani,” alisisitiza.