Mratibu Manywele Cup awapa mbinu wachezaji kumfikia Samatta

Dar es Salaam. Mratibu wa Mashindano ya soka Kata ya Kijichi, Mbagala jijini Dar es Salaam,  Michael Mwanswila ‘Manywele’, amewataka vijana Wilaya ya Temeke kuiiona fursa ya michezo kama kazi zingine za kuwaingizia kipato kwa kuweka nidhamu kwenye mazoezi.

Manywele alisema vijana wa Temeke wanafursa ya kufika mabali kutokana na kuwapo mtangulizi wao Mbwana Samatta ambaye alikuwa akicheza soka la mchangani akiwa Mbagala.

Aliongeza kuwa Samatta amefanikiwa kufika mbali kutokana na juhudi zake pamoja na nidhamu ya mazoezi na kusisitiza waendelee kumtazama kama kioo chao ili kuyafikia mafanikio.

Mwanswila aliyasema hayo wakati wa Mashindano ya Manywele Cup yaliyofikia tamati mwishoni mwa wiki hii katika fainali huku Aluminium FC wakiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Atletico FC mchezo uliopigwa viwanja vya Kwa Mbaraka.

Hata hivyo, Manywele alisema mashandano hayo yamekuwa na kaulimbiu ya kupinga uhalifu kwa vijana wanaotoka kwenye maeneo ili kuimarisha usalama wa maeneo yao.