Arsenal, Chelsea zavurugiana Kombe la Carabao

Thursday January 11 2018

 

England. Mechi ya jana Jumatano usiku uliowakutanisha Chelsea na Arsenal ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana  ikiwa ni mechi ya kwanza ya nusu fainali huku mastaa Mesut Ozil na Alexis Sanchez wakikosekana kikosi cha kwanza.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkali, inakuwa ni sare ya pili kwa Arsenal ndani ya wiki moja  ambapo awali walitoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Norwich kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la FA.

Kutokana na timu hizo kucheza mpira wa ushindani, lakini hakukuwa na dalili kwa upande wowote kushinda kutokana na kila upande kuzuia hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Stamford Bridge nyota, Alexis Sanchez hakucheza kwenye kikosi hicho cha Kocha Arsenal Wenger kwani aliitazama mechi hiyo akiwa bechi la timu hiyo.

Awali, ilielezwa kwamba mchezaji huyo yupo mbioni kujiunga na Manchester City, hivyo kocha wake kutokumchezesha, wachambuzi wanadhani huenda hiyo ni sehemu ya kumuaga.