Alliance Queens yaichapa Simba Queens

Muktasari:

Ligi hiyo inashirikisha timu nane za wanawake kutoka katika mikoa mbalimbali

Mwanza. Bao la Aisha Juma limetosha kuipa Alliance Queens ushindi mwembamba goli 1-0 dhidi ya Simba Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake.

Mchezo huo wa raundi ya nne umepigwa leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ulishudia wenyeji wakisubili hadi dakika 18, kupata ushindi huo kwa bao la Aisha na kuwafanya Alliance kufikisha pointi saba baada ya mechi nne, huku Simba Queens ikiwa na pointi tatu.

Kipindi cha kwanza wenyeji walitawala na kuwazidi wapinzani wake, huku wakitengeneza nafasi kadhaa na kushindwa kuzitumia vyema.

Licha ya Simba kubadirika kipindi cha pili kwa kulishambulia lango la Alliance, haikuweza kufanikiwa kusawazisha bao hilo hadi dakika 90 zinakamilika.