Abdulrahaman Mussa tatizo lake dogo tu!

Muktasari:

Abdulrahaman anapenda kuvaa jezi namba 17,  alicheza katika mechi yao dhidi ya Yanga wakafungwa bao 1-0, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

MASHABIKI wengi wa soka wanajiuliza maswali mengi juu ya kiwango cha mshambuliaji wa Ruvu

Shooting, Abdulrahaman Mussa kuwa kimeshuka, lakini kocha mkuu wa kikosi hicho, Abdulmutik

Haji amefafanua na kusema,  majeruhi ndiyo yamesababisha.

Abdulrahman alikuwa moto kwenye safu hiyo ya ushambuliaji msimu uliopita hadi akamaliza akiwa

kinara wa mabao kwenye msimamo wa ligi akifunga 14 sawa na ya Simon Msuva aliyekuwa

anaichezea Yanga.

Kocha huyo amesema: "Ni kweli Abdulrahaman hayuko sawa katika kipindi hiki, hajarudi kwenye

kiwango chake nafikiri yote ni kwa sababu anatoka kwenye majeruhi. Alikuwa mgonjwa na sasa ndiyo

anarudi taratibu."

Abdulrahaman anayependa kuvaa jezi namba 17,  alicheza katika mechi yao dhidi ya Yanga

wakafungwa bao 1-0, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.