Yanga yaitimulia vumbi Simba Kombe la Mapinduzi

Muktasari:

  • Yanga imerekebisha makosa baada ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu kwa kufungwa na timu ya Mbao FC Jumapili iliyopita.

Zanzibar. Kikosi cha Yanga kimeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuizamisha Mlandege mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaan jana Jumanne usiku.

Mabao ya Yanga katika mechi iliyochezwa kwenye mashindano hayo ya Kombe la Mapinduzi alikuwa ni Juma Mahadhi aliyefunga mabao yote wawili.
Awali, mechi ya Simba na Mwenge iliisha kwa sare ya bao 1-1 jambo linawapa presha Wekundu wa Msimbazi kuhakikisha wanafanya vyema mechi zinazofuata.