Manara apiga vijembe Kwa Yanga

Muktasari:

  • Manara alisema kuwa wao ndio klabu ya kwanza kupanda ndege, kuvaa viatu, hivyo wanahitaji kusogea mbele zaidi ya watani zao na kufanya mambo makubwa na kuwaacha midomo wazi watani zao.

Dar es Salaam. Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amewapiga vijembe watani zake wa jadi Yanga kwa kusema kuwa wanaenda kwenye mabadiliko ya juu zaidi, huku wao wakiwa wanaendelea kuwa nyuma.

Manara alisema kuwa wao ndio klabu ya kwanza kupanda ndege, kuvaa viatu, hivyo wanahitaji kusogea mbele zaidi ya watani zao na kufanya mambo makubwa na kuwaacha midomo wazi watani zao.

Manara pia kupitia mabadiliko hayo alisema wameanzia katika App yao ya Simba App ambayo inakuwa inaweka taarifa zao kamili ikiwa ni klabu ya kwanza kuwa na App yao kwa hapa nchini.