Chirwa aing'arisha Yanga

Muktasari:

  • Chirwa, Mchezaji Bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Oktoba, amefunga mabao matatu dakika ya 19, 49 na 59, wakati Emmanuel Martine alifunga mawili dakika ya 22 na 80 na kufanya matokeo kuwa 5-0.

STRAIKA wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa ameendelea 'kung'ara' katika Ligi Kuu Bara baada ya kufunga 'Hat -trick' yake ya kwanza msimu huu kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbeya City, jana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Chirwa, ambaye ni Mchezaji Bora wa Kigi Kuu kwa mwezi Oktoba, alifunga mabao hayo dakika ya 19, 49 na 59, wakati Emmanuel Martine alifunga mawili dakika ya 22 na 80 na kufanya matokeo kuwa 5-0.

Hiyo ni Hat-trick ya kwanza kwa Chirwa tangu aliposajiliwa na Yanga msimu uliopita na hat-trick ya pili msimu huu, ya kwanza ikifungwa na Emmanuel Okwi wa Simba.

Katika mchezo huo uliochezwa uwanjani hapo, Yanga walicheza kwa umakini na kupata matokeo hayo yanayowabakisha nafasi ya tatu na pointi 21, nyumba ya Simba inayoongoza na pointi 22 ambazo ni sawa na za Azam wanaoshika nafasi ya tatu.

Matokeo ya mechi nyingine, Azam imewatambia Njombe Mji kwao baada ya kuwachapa bao 1-0, lililopachikwa na Aggrey Morris.

Wakata miwa wa Mtibwa Sugar, wameshindwa kutamba kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Manungu, Morogoro, wakichapwa kwa bao 1-0 na Kagera Sugar, lililofungwa na Edward Christopher katika dakika 85.

 

Kikosi cha Yanga

1 Youth Rostand, 2 Juma Abdul, 3Gadiel Michael, 4 Andrew Vincent, 5Nadir Haroub 'Cannavaro', 6Pato Ngonyani, 7 Pius Buswita, 8Raphael Daud, 9Obrey Chirwa, 10Ibrahim Ajib/Geofrey Mwashiuya, 11Eammanuel Martine.