Simba yawaita mashabiki kuizima Djibouti

Muktasari:

Simba ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyofanikiwa kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 1993

Dar es Salaam. Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi yao ya Jumapili ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba watacheza mechi ya kimataifa dhidi ya Gendermerie kutoka Djibouti katika mechi ya kwanza Kombe la Shirikisho ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Manara alitangaza viingilio katika mechi hiyo na itakuwa VIP ''A' Sh 30000, VIP 'B' Sh 20000, Viti vya Orange sh 10000, na mzunguko Sh 5000.

Manara alisema anawaomba mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao yenye ni madhubuti kupata ushindi mkono kwenye pambano hilo.

"Tunakiu ya kufanya vizuri katika ligi hata michuano hii ya kimataifa mashabiki waje kuishangiria timu yao na tunawahidi hatutawaangusha," alisema Manara.