Mashabiki wamtuhumu meneja wa Diamond Platnumz

Meneja wa msanii wa muziki Diamond Platnumz, Sallam SK ametupiwa dongo  na mashabiki kuacha tabia ya kuhamishia bifu za watu kwa Mwanamuziki wake Diamond.
    Sallam amedaiwa kuwa na tabia ya  kuzima skendo za wanamuziki wa Wasaf (WCB) kwa kile kila kinachotokea hupenda kusema kauli ya 'Yote yanayotokea ni kwa ajili ya Diamond kutaka kupotezwa kwenye Muziki' hata kama wanamuziki hao wamefanya kosa, yeye hupoteza kwa kumtanguliza Diamond.
Hivi karibuni ilitokea inshu ya mnenguaji wa Diamond ,Moses Iyobo kwenda kuhojiwa na Shilawadu lakini alishindwa kutoa ushirikiano na matokeo kudaiwa kufanya uharibifu wa vifaa vya kazi na kutishia kutaka kuwagonga na gari (video zipo zinaonyesha).
   Lakini baada ya hapo Shilawadu wakaenda kutoa taharifa polisi kwa ajili ya uharibifu wa vifaa ili waweze kulipwa,na walisema hawakuwa na mpango wa kwenda kumbeba Moses Iyobo kwani walijua watakaa chini na kuyaongea kwani ni watu ambao wanafahamiana.
Kwa habari zilizozagaa na kipande cha video kinaonyesha Moses Iyobo alikamatwa na kupelekwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbey,lakini baadae alitolewa.
Sasa kwa upande wa Sallam amedai kwamba tukio hilo ni sababu moja wapo ya kumshusha mwanamuziki Diamond na ameweza kuandika katika ukurasa wake wa kuwa:
   “Kumbe tatizo ni kumpoteza huyu kijana? Waambie familia yako na wazazi waliokuleta katika haya maisha huyu mtoto kaletwa kwa makusudi maisha haya, ili kuleta ukombozi ya dhulma uliyokuwa unaleta kwenye Taifa hili ...,” aliandika Sallam kupitia instagram yake.
Pia kwa habari ambazo zipo mtaani zinadai kwamba wasanii wa WBC hawapati 'airtime' kama kipindi cha nyuma hali ambayo inatishia biashara ya wasanii hao na kuna baadhi ya vituo vya redio na runinga vitatu havipigi nyimbo hizo na wala hawaendi kutambulisha nyimbo zao mpya.