Kundi la Ingazo Ngari lawasha moto Zanzibar

Muktasari:

  • Tamasha hilo linaendelea katika eneo la Ngome Kongwe, visiwani Zanzibar

Kundi la ngoma za Asili kutoka nchini Rwanda, Inganzo Ngari usiku wa kuamkia jana Februari 10, 2018 wamewasha moto wa burudani katika jukwaa kubwa la Tamasha la Kimataifa la Muziki Sauti za Busara 2018.

Tamasha hilo ambalo limekuwa kivutio kwa wageni, linaendelea katika eneo la Ngome Kongwe, visiwani Zanzibar.

Kila mwaka Tamasha la Sauti za Busara limekuwa likiwakutanisha wasanii kutoka kila pembe ya dunia na kupanda jukwaa moja.

Vikundi mbalimbali vya asili na wasanii kutoka nchi tofauti walipata nafasi ya kupanda kwenye jukwaa mwaka huu.