SIRI imefichuka kwamba Matonya ameuza nyumba yake ya jijini Tanga, lakini amewaambia marafiki zake wa karibu kwamba amefanya hivyo ili mambo yaende sawa kimaisha na siku si nyingi ataibukia kwingine.
STAA wa muziki wa Bongo anayekubalika Mombasa, Husein Machozi, anakaribia kukamilisha video yake ya wimbo wa Jela lakini amelalamikia kupanda kwa gharama za maisha na kurekodi huku akisisitiza Serikali kuchukua hatua
MAGWIJI wa soka nchini, Gor Mahia, wanaohaha kurejesha ubabe wao, leo Jumamosi wana kibarua cha kujaribu makucha watakayoyatumia katika mashindano ya Afrika kwa kuvaana na El Mereikh ya Sudan.
TIMU ya taifa ya soka ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17, Jumamosi ijayo itakuwa na kibarua kigumu cha kuishinda Nigeria kwenye mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia.